Berlin . Matokeo ya sare yaleta mtafaruku wa kisiasa.
19 Septemba 2005Uchaguzi mkuu wa bunge nchini Ujerumani umemalizika kukiwa hakuna mshindi, na kuiingiza nchi hiyo katika hali ya kutokuwa na hakika kisiasa.
Matokeo ya mwanzo yalikipa chama cha Christian Democratic Union, kinachoongozwa na Angela Merkel, pamoja na chama ndugu cha jimbo la bavaria cha Christian Social Union ,asilimia 35.2 ya kura .
Chama cha kansela Gerhard Schröder cha Social Democrats kimepata asilimia 34.3.
Matokeo hayo yanakipa chama cha CDU, ambacho kilianza kampeni kikiwa kinaongoza katika kura ya maoni kwa asilimia 21, viti vitatu zaidi katika bunge la shirikisho, Bundestag.
Washirika wakuu wa CDU katika kuunda serikali , chama cha Free Democrats wamepata asilimia 9.8 ya kura na kushindwa kupata wingi wa kutosha kati yao unaotakiwa kuweza kuunda serikali.
Chama kidogo katika muungano wa serikali unaoongozwa na Bwana Schröder, chama cha Green kimepata asilimia 8.1, ambayo pia haitoshi kwa muungano huo kuweza kuunda serikali.
Chama kipya cha Linkepatai, au Left party kimepata asilimia 8.7.