BERLIN: Majadiliano yataendelea kuhusu mradi wa kinuklia wa Iran
26 Juni 2005
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer amesema anataraji kuwa Ujerumani,Ufaransa na Uingereza zitaendelea kujadiliana na Iran kuhusu mradi wake wa kinuklia,hata baada ya Mahmoud Ahmedinejad kuchaguliwa kama rais mpya wa nchi hiyo.Lakini ametoa mwito kwa Iran ihakikishe kuwa,mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizi ya amani tu kama inavyodaiwa na serikali ya Teheran.Kwa wakati huo huo ameeleza wasi wasi wake kuhusika na utaratibu wa uchaguzi uliofanywa akisema kuwa kulikuwepo dosari fulani.Msemaji wa serikali ya Marekani vile vile alieleza wasiwasi wa Washington kuhusu uchaguzi wa Iran,akinukulu madai kuwa kulifanywa udanganyifu wa uchaguzi na kwamba zaidi ya watu 1,000 waliotaka kugombea uchaguzi walipigwa marufuku.