BERLIN : Maelfu ya Wajerumani kuhudhuria kutawazwa kwa Papa mpya
23 Aprili 2005Matangazo
Wajerumani wanaofikia 100,000 wanatarajiwa kusafiri kwenda Rome nchini Italia hapo kesho kumuona Joseph Ratzinger akitowa misa yake ya kutawazwa kama Baba Mtakatifu Benedikt wa Kumi na Sita.
Kansela Gerhard Schroeder na Rais Horst Koehler wa Ujerumani pia watakwenda Rome kuungana na viongozi wa dunia katika seherehe hizo.Takriban watu lakini tano wanatazamiwa kufurika uwanja wa St. Peter hapo kesho.
Mapema hapo jana papa huyo amekuwa na mkutano wake wa kwanza na makadinali wa Kanisa Katoliki huko Vatican na kusema kwamba anataka kutumika badala ya kutukuzwa wakati wa uongozi wake kama papa.