BERLIN: Madola makuu yajadili mgogoro wa Iran
8 Septemba 2006Matangazo
Ujerumani na nchi tano zilizo wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa zimekutana mjini Berlin kujadiliana njia ya kuutenzua mgogoro wa kinuklia wa Iran. Haijulikani ni maendeleo gani yaliyopatikana, lakini mwanadiplomasia mmoja wa Ulaya amesema, majadiliano hayo yalifuata mwongozo wa azimio 1696 la Baraza la Usalama.Azimio hilo limesema uwepo uwezekano wa kuiwekea Iran vikwazo ikiwa mradi wake wa kurutubisha uranium hautositishwa kufikia tarehe 31 Agosti.Huu ni mkutano wa kwanza kupata kufanywa na madola hayo sita makuu tangu kumalizika kwa wakati huo uliodharauliwa na Iran.