BERLIN: Madaktari wafanya mgomo hapa Ujerumani
1 Agosti 2005Matangazo
Madaktari 1,400 wameanza mgomo wao hii leo ikiwa ni siku ya kwanza ya maandamano ya wiki moja kupinga mda mrefu wa kufanya kazi na kupunguzwa kwa mishahara. Shirika la madaktari hapa Ujerumani, Marburger Bund, limesema madaktari elfu 146 hutumikia saa milioni 50 za ziada kila mwaka.
Limesema pia kwamba mishahara wanayolipwa ni nusu au thuluthi moja ya mishahara ya wenzao wa Ufaransa, Uingereza na Marekani. Siku hizi wanalazimika kufanya kazi kwa saa 42 kwa wiki huku marupurupu ya likizo na sherehe ya Krismasi yakiwa yamefutiliwa mbali.