BERLIN :Maandamano kupinga mpango wa kubana matumizi
6 Novemba 2005Maalfu ya watu jana waliandamana mjini Berlin kupinga walichoita serikali ya mseto ya wizi wa kijamii.
Maalfu ya watu hao wameandamana wakati ambapo wajumbe wa vyama vikuu vya siasa wanafanya mazungumzo juu ya kuunda serikali ya mseto itakayokabiliwa na jukumu la kupunguza pengo katika bajeti, la kiasi cha EURO bilioni 35.
Pamoja na hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa ili kupunguza pengo hilo ni kukata posho za watu wasiokuwa na ajira.
Wakati huo huo wawakilishi wa vyama vikuu kwenye mazungumzo yao ya kuunda serikali ya mseto wanapingana juu ya hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kupunguza nakisi hiyo ya Euro bilioni 35.
Wakati chama cha CDU kinataka kuongezwa kwa kodi ya mauzo , chama cha SDP kinatetea hoja ya kuwatoza kodi zaidi watu wenye vipato vya juu.