BERLIN: Maandamano kama kawaida wakati wa mei dei.
2 Mei 2005Sherehe za mei mosi zilikumbwa na misukosuko hapo jana mjini Berlin na polisi wa kupambana na ghasia walikabiliwa na wakati mgumu kukabiliana na waandamanaji wa mrengo wa kushoto na vile vile hali kama hiyo katika mji wa Leipzig mashariki mwa Ujerumani.
Msemaji wa polisi amesema kuwa maafisa watatu walipata majeraha madogo katika tukio hilo, hata hivyo utawala umesema kuwa maandamano hayo ya jana hayakuwa makubwa yakilinganishwa na wakati kama huo mwaka jana ambako watu 200 walijeruhiwa na wengine 200 walitiwa mbaroni.
Maandamano kama hayo yamekuwa ni jambo la kawaida katika mji mkuu wa Berlin.
Kwengineko siku ya wafanyakazi duniani iliadhimishwa ulimwenguni kote hapo jana, zaidi ya watu millioni walikusanyika mjini Havana nchini Cuba kuadhimisha siku hii.