BERLIN: Maafisa wa Kijerumani kusadia ukaguzi wa abiria na mizigo
7 Septemba 2006Matangazo
Serikali ya Ujerumani inajitayarisha kwa ujumbe wa kupeleka vikosi vyake nchini Lebanon.Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier hii leo anakwenda Beirut.Waziri huyo anakwenda pamoja na walinzi wa mipaka na maafisa wa forodha kusaidia kulinda usalama kwenye uwanja wa ndege wa Beirut.Alipozungumza na waandishi wa habari mjini Istanbul nchini Uturuki,Steinmeier alisema maafisa 10 wa Kijerumani watasaidia kuwakagua abiria na mizigo kwenye uwanja wa ndege wa Beirut.Lengo ni kupunguza uwezekano wa kuingizwa silaha za magendo kwa wanamgambo wa Hezbollah.Bado haijulikani lini baraza la mawaziri la Ujerumani litakutana rasmi kupitisha uamuzi ikiwa ipeleke manowari zake za kijeshi kwenye mwambao wa Lebanon.