BERLIN :Kumbukumbu ya miaka 60 ya ukombozi wa Belsen
16 Aprili 2005Matangazo
Wahanga walionusurika na Maangamizi ya Wayahudi wamekuwa na kumbukumbu ya miaka 60 ya kukombolewa kwa kambi ya mateso ya Bergen-Belsen.
Kambi hiyo iliokuwa karibu na mji wa kaskazini wa Ujerumani wa Hanover ilikombolewa tarehe 15 mwezi wa April mwaka 1945.Hiyo ilikuwa ni kambi ya kwanza ya Manazi kukombolewa na wanajeshi wa Uingereza.Ibada kuu ya kumbukumbu imepangwa kufanyika huko Bergen-Belsen hapo kesho.
Watu wanaokadiriwa kufikia 70,000 wamekufa kwenye kambi hiyo kutokana na utapia mlo na magonjwa kama vile homa ya matumbo na kifua kikuu.