BERLIN Kesi ya utoaji visa yaanza kusikilizwa tena
16 Juni 2005Matangazo
Kamati ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji visa, inayomkabili waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, imerudia vikao vyake hii leo, licha ya juhudi za serikali kuumaliza uchunguzi huo. Mahakama hiyo imesema hatua ya serikali kusimamisha kusikilizwa kwa kesi hiyo ilikuwa kinyume cha sheria.