BERLIN: Katika Ziara ya Bush Barani Ulaya
23 Februari 2005Rais Gorge Bush wa Marekani amewasili mjini Mainz nchini Ujerumani katika ziara yake barani ulaya.Bush atafanya mazungumzo na Kasella wa Ujerumani Gerhard Schroeder.
Mjini Brussels Bush alitaja dhana kwamba Marekani inampango wa kuivamia Iran kuwa ya kudhihaki. Akizungumza baada ya mkutano maalum na viongozi wa umoja wa Ulaya ,hata hivyo alisema kwamba uhuru wa kuchagua unabakia wazi kwa Iran.
Tofauti ziliendelea kutanda katika ziara yake hiyo Gorge Bush huku rais wa Ufaransa Jacque shirac akitaka suala la iran litatuliwe kidiplomasia.
Upande wake rais Bush alionya dhidi ya biashara ya silaha na China.Hata hivyo Umoja wa Ulaya na Marekani zimekubaliana katika mkutano wa hapo jana juu ya kuijenga upya Iraq huku NATO ikiahidi kusaidia kutoa mafunzo kwa vikosi vya usalama vya Iraq.