BERLIN. Kansela wa Ujerumani kutoa hoja za kufufua uchumi wa Ujerumani.
17 Machi 2005Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröeder leo anatarajiwa kutoa hoja ya njia za mageuzi katika mfumo wa kodi ya mapato pamoja na hatua zingine za kufufua uchumi.
Kansella Schröeder atalihutubia bunge na kutoa muelekeo wa mikakati ya chama cha SPD na kuanzisha rasmi agenda ya kufufua uchumi tangu miaka miwili iliyopita hadi mwaka 2010.
Wadadisi wa kiuchumi wanaona kama hatua ya kansela Gerhard Shcröeder inamuelekeo wa kutafuta kuungwa mkono upya baada ya kura ya maoni kuonyesha kuwa chama chake cha SPD kimepoteza wafuasi baada ukosefu wa ajira kukithiri nchini Ujerumani na kupanda kwa bei ya mafuta.
Baadae kansela Schröeder atakutana na viongozi wa upinzani bibi Angela Merkel na Edmund Stoiber.
Hapo jana rais wa shirikisho la Jamuhuri ya Ujerumani Horst Köhler aliihimiza serikali na upande wa upinzani wazidishe juhudi za pamoja kupambana na ukosefu wa ajira.