BERLIN. Kansela wa Ujerumani ateta juu ya bei kubwa ya mafuta
7 Septemba 2005Matangazo
Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani amelaumu kiasi kikubwa cha faida kinachochukuliwa na makampuni makubwa ya mafuta kutokana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo ulimwenguni.
Kansela Gerhard Schröder amekemea bei hizo za juu ambazo amesema ipo haja ya kufanyiwa marekebeisho na wakati huo huo ameonya juu ya athari ya kupanda kwa bei ya mafuta ulimwenguni baada ya kimbunga cha Katrina nchini Marekani.
Ujerumani imetoa mapipa milioni 3.3 ya mafuta kutoka kwenye akiba yake kuisaidia Marekani baada ya kimbunga hicho na hii ni kwa mujibu wa makubaliano ya nchi 26 wanachama wa bodi ya kimataifa ya nishati.