BERLIN: Kansela mteule wa Ujerumani Merkel aeleza matumaini juu ya serikali ya mseto
28 Oktoba 2005Matangazo
Kansela mteule wa Ujerumani bibi Angela Merkela amesema anatumaikwamba chama chake CDU na chama cha SD vitafikia lengo la kuunda serikali ya mseto hadi kufikia katikati ya mwezi ujao.Bibi Merkel amesema, kwamba licha ya kuwepo vizingi virefu,mazungumzo juu ya kuunda serikali hiyo yanaendelea.
Sambamba na suala la kuunda serikali ya mseto,pande mbili hizo zimepitisha uamuzi juu ya kurekebisha bajeti ya nchi. kwa kubana matumizi ili kuziba pengo la Euro bilioni 35 katika bajeti ya nchi. Hatua za kufikia shabaha hiyo ni pamoja na kupandisha kodi ya mapato na kupandisha umri wa kustaafu .