BERLIN: Kansela Merkel ametetea matamshi ya Papa
16 Septemba 2006Matangazo
Kansela Angela Merkel na viongozi wengine wa kisiasa nchini Ujerumani,wameitetea hotuba ya utata iliyotolewa na Baba Mtakatifu Benedikt wa 16.Katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani “Bild”,Merkel amesema matamshi ya Papa yameelewa visivyo.Kiongozi wa chama cha CSU,Edmund Stoiber amesema yeye haoni sababu ya kukosoa matamshi ya Papa.Lakini mkuu wa Halmashauri Kuu ya Waislamu nchini Ujerumani,Ayyub Axel Köhler ametoa wito wa kuombwa radhi rasmi.