Berlin. Kansela apuuzia barua ya rais wa Iran.
22 Julai 2006Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amepuuzia barua kutoka kwa rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad inayotaka ushirikiano na Ujerumani.
Kansela Merkel ameiambia televisheni ya umma ya Ujerumani kuwa barua hiyo inarudia mawazo yaliyoelezwa hapo kabla na rais Ahmedinejad, ambayo hayakubaliki kabisa na Ujerumani.
Amesema kuwa barua hiyo inaulizia uhalali wa kuwapo kwa Israel, kitu ambacho ni sehemu muhimu ya sera za mambo ya kigeni ya Ujerumani.
Merkel ameongeza kuwa barua hiyo haikutaja kabisa pendekezo lililotolewa na Ujerumani na mataifa mengine ya kimagharibi lenye lengo la kutanzua mkwamo baina ya Tehran na mataifa hayo ya magharibi juu ya mpango wake wa kinuklia.