BERLIN: Jung amekamilisha ziara yake barani Afrika
27 Septemba 2006Matangazo
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung amekamilisha ziara yake ya siku tatu barani Afrika na amerejea Berlin.Alipokuwa Kinshasa, aliiahidi Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kuwa Ujerumani itaendelea kuisaidia nchi hiyo hata baada ya mwezi wa Novemba.Mifano ya misaada hiyo amesema ni kama kutoa mafunzo ya kijeshi na misaada ya maendeleo.Wakati huo huo akasema,muda wa vikosi vya Ujerumani kubakia Kongo hautorefushwa.Ujerumani imetoa mchango wa kama wanajeshi 780 kulinda usalama wakati wa uchaguzi nchini Kongo.Vikosi hivyo vile vile vitalinda usalama wakati wa kufanywa duru ya pili ya uchaguzi wa rais wa Kongo.Rais wa hivi sasa Joseph Kabila atapambana na makamu wake Jean- Pierre Bemba mwisho wa mwezi Oktoba.