BERLIN: Jumblatt akutana na Fischer
9 Machi 2005Matangazo
Kiongozi wa chama cha upinzani "Druze" nchini Lebanon,Walid Jumblatt amekuwa na mazungumzo mjini Berlin pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer.Katika mkutano wa pamoja na waandishi habari,Jumblatt ametoa muito kuwa vikosi vya Syria viondoshwe kwa utaratibu kutoka Lebanon.Fischer amemuarifu Jumblatt kuwa serikali ya Berlin inaunga mkono juhudi za Lebanon kuleta demokrasia zaidi na ametoa muito kwa Damascus iviondoshe vikosi vyake vyote kutoka Lebanon.