BERLIN. Joscka Fischer kushuhudia mbele ya kamati ya bunge.
1 Aprili 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani bwana Joschka Fischer, atashuhudia mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji viza mwezi ujao. Anatarajiwa kuyajibu maswali kuhusiana na jukumu lake katika kashfa hiyo. Waziri huyo hakutarajiwa kushuhudia mpaka baada ya uchaguzi wa mkoa wa North-Rhine Westfalia kufanyika mwezi Mei, lakini upinzani umepigania Fischer ashuhudie kabla uchaguzi huo.