BERLIN: Janga la kiutu katika Ukanda wa Gaza
9 Julai 2006Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan,ametoa mwito kwa serikali ya Israel,kutozuia huduma za wafanya kazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika yanayotoa misaada ya kiutu katika Ukanda wa Gaza.Annan amesema,hatua ya dharura ichukuliwe kupunguza kile alichokiita “hali mbaya sana ya kiutu” inayokabiliwa na raia wa kawaida.Akaeleza kuwa mashambulio ya angani ya Israeli yameteketeza kinu pekee cha umeme katika Ukanda wa Gaza na kuathiri hospitali,viwanda vya kusagia unga na mitambo ya maji.Annan ametoa mwito kwa serikali ya Israel ichukuwe hatua ya haraka kukifanyia ukarabati kinu cha umeme kilichobomolewa.