BERLIN: Israel yatuhimiwa kushambulia vituo vya kiraia
23 Agosti 2006Matangazo
Shirika linalogombea haki za binadamu duniani,Amnesty International,limeituhumu Israel kuwa kwa makusudi ilishambulia vituo vya kiraia wakati wa mapigano yake dhidi ya Hezbollah. Shirika hilo limetoa mwito kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza ikiwa Israel na Hezbollah zimekiuka haki za binadamu.