BERLIN: Idadi ya maombi ya hifadhi yapungua.
8 Aprili 2005Matangazo
Ripoti iliyochapishwa kutoka wizara ya mashauri ya ndani ya Ujerumani inasema kuwa idadi ya watu wanaowasilisha maombi ya hifadhi nchini Ujerumani imepungua kwa kiasi kikubwa.
Jumla ya watu 6,900 walituma maombi ya kutaka hifadhi katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu 2005 hapa Ujerumani kiasi hicho ni cha chini kwa thuluthi tatu ikilinganishwa na muda huo katika mwaka uliopita.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa zaidi ya waliotuma maombi ya kutaka hifadhi ni watu kutoka Serbia na Montenegro, Turki na Urusi.