BERLIN: Gebrselassie ameshinda mbio za marathon
24 Septemba 2006Matangazo
Mwana riadha mashuhuri Haile Gebrselassie kutoka Ethiopia,ameshinda mbio za masafa marefu-marathon mjini Berlin.Miongoni mwa wanawake,Muethiopia Gete Wami alimshinda Mkenya Salina Kosgei aliechukua nafasi ya pili.Zaidi ya watu 40,000 walishiriki katika mbio hizo za marathon leo hii katika mji mkuu wa Ujerumani.