BERLIN: Fischer kujieleza kuhusu kashfa ya viza
2 Aprili 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Joschka Fischer mwezi ujao atafika mbele ya halmashauri maalum ya uchunguzi.Fischer atakhojiwa kuhusu ile kashfa ya viza zilizotolewa katika balozi za Ujerumani nchini Ukraine na nchi zingine za Ulaya ya mashariki.Vyama vya kikonsavativ vya upande wa upinzani nchini Ujerumani vinasema sheria za viza zilizoregezwa katika nchi hizo,ziliyarahisishia makundi ya wahalifu kufanya magendo ya kuingiza watu nchini Ujerumani na nchi zingine za Ulaya.