BERLIN. Fischer ashuhudia mbele ya kamati ya bunge kuhusu kashfa ya utoaji visa.
25 Aprili 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Joschka Fischer, ameanza kushuhudia mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kashfa ya utoaji visa. Hii ni mara ya kwanza kwa ushahidi unaotolewa na waziri wa serikali ya kansela Gerhard Schroeder kuonyeshwa moja kwa moja katika runinga humu nchini.
Fischer anakabiliwa na maswali kuhusu kulegeza kamba sheria za utoaji visa zilizoanza kufanya kazi miaka mitano iliyopita. Upinzani unasema sheria hizo ziliyaruhusu makundi ya wahalifu kuwaingiza wahamiaji haramu nchini Ujerumani kutoka Ulaya mashariki. Ushahidi wa Fischer unatarajiwa kuchukua kipindi kirefu katika shughuli za leo za kamati hiyo.